
Mshambliaji wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Uganda,Emmanuel Okwi mwishoni mwa juma hili alifunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Nakalega Florence.
Ndoa hiyo ilifungwa mwishoni mwa juma hili nchini Uganda na kuhudhuliwa na ndugu jamaa na marafiki.
Akizungumza kutoka Kampala, Uganda, Okwi alisema amefanya hivyo kutokana na heshima kubwa pia anayoipa klabu yake ya Simba.
"Kweli nimeamua kukatisha fungate, nitarudi Dar es Salaam kuiwahi mechi ya ligi kuu dhidi ya Kagera.
"Baada ya hapo nitaomba ruhusa ili nirudi kuendelea na ratiba ya fungate," alisema.
"Natamani kushirikiana na wenzangu kwa kuwa najua tunahitaji pointi tatu za Kagera, ni timu ngumu na umoja wetu unahitajika," alisema.
Okwi amefunga ndoa ya kimila, halafu ndoa ya dini ya Kikristo itafungwa Julai, mwakani.
