Beki wa Simba Joram Mgeveke amejiunga na Mwadui FC kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu huu,
Akiongea na mtandao wa www.shaffihdauda.com makamu wa rais wa Simba Geoffrey Kaburu amesema wamefunga rasmi usajili usiku huu kwa kumsajili beki wa kulia wa Mtibwa Sugar Hassan Kessy kwa mkataba wa miaka miwili,
Wakati wakimalizia usajili wa Kessy pia amesema wamevunja mikataba na wachezaji watatu ambao ni Uhuru Selemani,Amis Tambwe na kiungo Piere Kwizera na tayari wameshamalizana.
Wakati huo huo klabu hiyo imewatoa kwa mkopo wachezaji wake watau kwenda vilabu mbali mbali,wachezaji hao ni Haruna Chanongo alikwenda Stand Utd,Miraji Adam aliyekwenda Mtibwa Sugar akiwa sehemu ya uhamisho wa Hassan Kessy pamoja na beki Joram Mgeveke alipelekwa Mwadui FC.

Advertisement

 
Top