Mechi
ya Nani Mtani Jembe namba 2 itafanyika kesho siku ya jumamosi katika dimba la
Uwanja ambapo itawakutanisha Young Africans Sports Club dhidi ya Simba SC huku
timu zote zikitarajiwa kuwatumia wachezai wao wapya zilizowasajili katika
kipindi cha dirisha dogo.
Kikosi cha mbrazil Marcio Maximo tayari kimeshawasajili wachezaji
wawili kiungo Emerson de Oliveira kutoka nchini Brazil na mshambuliaji mkongwe
na mzoefu wa hali ya juu Danny Mrwanda ambao wanatajiwa kuongeza nguvu katika
mchezo huo wa kesho.
Young Africans chini ya kocha mkuu Marcio Maximo inaendelea na
mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterani huku wachezaji wote 26 waliongia
kambini wakiendelea kujifua kuwa fit kwa ajili ya mchezo huo wa siku ya
jumamosi.
Huu ni mchezo wa pili wa Nani Mtani Jembe kuzikutanisha timu hizi
kwani katika mchezo wa awali uliofanyika mwaka jana, Young Africans ilipoteza
kwa mabao 3- 1, na kocha Maximo pamoja na wachezaji wake wamejiandaa
kuhakikisha safari hii wanapata ushindi kwenye mchezo huo.
Kocha Maximo amesema vijana wake wote wapo kwenye hali nzuri
kuelekea mchezo huo, ambapo mchezaji pekee majeruhi ni Jerson Tegete ambaye
alipata majeraha hayo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Vipers kutoka
nchini Uganda.