Chelsea na PSG, zitakuwa zinakumbushia robo fainali ya msimu uliopita, na Chelsea ikiiondosha PSG, kwa bao la ugenini, baada ya Chelsea kuibuka na ushindi wa nyumbani wa mabao 2-0, kabla ya kubandikwa mabao 3-1, jijini Paris nchini Ufaransa, lakini bao la ugenini likaivusha..sijui safari hii…
Vita nyingine kubwa safari hii hatua ya robo fainali, ni Manchester City itakapokuwa inapoma ubavu dhidi ya kigogo FC Barcelona ya Hispania, hapa tunaweza kuipima Man City kutokana na utajiri wa kikosi chake, dhidi ya uzoefu wa Barca,,ambayo kama si kufanya yake, mara zote huishia katika hatua za juu…


Wenger anakumbushia urejeo wake kwenye jiji la Monaco, akifundisha AS Monaco, wana fainali wa Champions league wa msimu wa 2003/04..pale Arsenal itakapokuwa ikikabiliana na AS Monaco ya Ufaransa..
Kazi nzito wanayo Shakhter ya Ukrain, ambao mbele yao watakuwapo Bayern Munich ya Ujerumani..nao Shalke wa Ujerumani wakiangukia mikononi mwa mabingwa watetezi wa taji Real Madrid ya Hispania, lakini Juventus na Borussia Dortmund nazo zikikumbushia fainali ya mwaka 1997..
