Kocha Mkuu wa Simba, Mzambia Patrick Phiri amesema jijini hapa leo kuwa kikosi chake kitaingia kambini kesho kwenye Hoteli ya Ndege Beach na baadaye Jumapili kitarejea Visiwani Zanzibar kuandaa dozi kwa ajili ya kukiua kikosi cha kocha Mganda Jackson Mayanja cha Kagera Sugar kilichoifunga Yanga bao 1-0 katika mechi ya raundi ya sita ya VPL msimu huu.
Aidha, Kikosi cha Simba kitacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mwadui FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL). Mechi hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini hapa Jumamosi.
Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ aliyewahi kuinoa Simba SC ametamba kufanya vizuri katika mechi hiyo.
Simba iko nafasi ya saba katika msimamo wa VPL ikiwa na pointi tisa, moja nyuma ya Kagera Sugar wanaokamata nafasi ya tano.
Simba SC imekuwa na utaratibu wa kuweka kambi Zanzibar kila inapokuwa inakabiliwa na mechi ngumu. Kabla ya kuc