Tayari kikosi cha Simba kipo mjini Mtwara kwa ajili ya mechi yake ya leo dhidi ya wenyeji wake Ndanda FC.

Wakati Ndanda wamejichimbia nje ya mji, wageni Simba ndiyo wametawala na walionyesha kwamba wanakubalika kutokana na idadi kubwa ya mashabiki waliojitokeza wakati wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Nangwana Sijaona.

Chini ya Kocha Goran Kopunovic Simba walijifua ili kujiweka sawa kwa ajili ya mechi hiyo ya kesho.


Advertisement

 
Top