Klabu ya Chelsea imetangaza kuingia mkataba na kampuni ya kuuza matairi ya magari ya Yokohama ya nchini Japan.
Kwa hapa nyumbani, kampuni ya Bin Slum Tyres ndiyo imekuwa iking’ara katika klabu za Ligi Kuu Bara ikiwadhamini Mbeya City, Stand United na Ndanda FC.
Msimu ujao, Chelsea itaanza kujimwaga Yokohama na kuachana na Samsung ambayo wamekuwa wakiitumia na mkataba wao unaisha mwishoni mwa msimu huu.
Yokohama itakuwa ikimwaga pauni milioni 40 kwa mwaka katika klabu hiyo inayomilikiwa na Mrusi, Roman Abramovich.
Mkataba wa Chelsea na Yokohama utakuwa wa miaka mitano na wa pili kwa ukubwa ukifuatiwa ule wa Manchester United na kampuni ya magari ya Chevrolot ambayo inamwaga pauni milioni 53 kwa mwaka.