IBRA AJIBU 'KADABRA' (KUSHOTO) AKIWANIA MPIRA NA MOHAMMED HUSSEIN 'TSHABALALA' KATIKA MAZOEZI YA SIMBA MJINI ZANZIBAR. |
Kocha
Goran Kopunovic wa Simba amesema mmoja wa wachezaji wake walio tayari kwa ajili
ya mechi dhidi ya Yanga, Jumapili ni mshambuliaji kinda, Ibrahim Ajib
‘Kadabra’.
Kinda
huyo alifunga mabao matatu 'hat trick' katika mechi iliyopita ya Ligi
Kuu Bara wakati Simba ilipoitwanga Prisons kwa mabao 5-0.
Kopunovic
amesema Ajib amekuwa akijifua vizuri na wenzake na anafurahi kuona kikosi ni kipana.
“Kikosi
kinakuwa kipana kama wachezaji wote wako fiti, unakuwa na nafasi ya kuchagua,”
alisema kocha huyo raia wa Serbia.
“Matumaini
ni makubwa kwa kuwa vijana furaha na wako tayari kwa ajili ya kupambana hiyo
Jumapili. Tunazihitaji sana pointi tatu.”
Simba imeweka kambi Zanzibar kujiandaa na mechi hiyo dhidi ya watani wake Yanga ambao wameweka kambi mjini Bagamoyo.