Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amewashangaa wanaoona kikosi chake hakiwezi kuwania ubingwa.

Kopunovic amesema wanaoamini Simba haiwezi kuwania ubingwa, wanajidanganya na watakuwa hawajui mambo ya mchezo wa soka.

“Zimebaki mechi sita kwetu, wengine wana saba au nane. Lakini mpira una mambo mengi ambayo hutokea bila ya wewe kuyatarajia.

“Angalia Yanga wana tofauti ya pointi tano dhidi yetu, wakishinda dhidi ya JKT ni point inane. Bado inawezekana kufanya kitu kwetu.

“Tunachotakiwa ni kufanya vizuri katika kila mechi iliyobaki, halafu wengine majibu yatapatikana lakini nisisitize, tuko kwenye mbio za ubingwa,” alisema Kopunovic.

Simba iko katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 32 huku Azam FC wakibaki nafasi ya pili na pointi 36.

Vinara wa ligi hiyo ni Yanga wakiwa na pointi 40, hivyo kufanya ushindani kuwa mkali kileleni.

Hata hivyo Simba ina michezo mingi zaidi ya Yanga na Azam kwa kuwa imecheza mchi 20.

Wakati Azam imecheza 18 na Yanga tayari imeshuka dimbani mara 19.

Advertisement

 
Top