
Mabondia Mohammed Matumla, kutoka Tanzania pamoja na Wang Xin Hua ambaye ni raia wa China, jana mchana wamepima uzito tayari kwa mhezo wao wa kimataifa wa Masumbwi utakao pigwa katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo
Wapiganaji hao kila mmoja ametoa
tambo zake pamoja na vitisho kwa mwenzake, ambapo Matumla ametamba kuwa
ni lazima amzimishe mpinzani wake huyo kutoka China, nae Hua akafunguka
na kusema haitakuwa lahisi na anachoamini Matumla atamkalisha kwa KO.
Mohammed amekuwa akinolewa baba
yake mzazi Rashid Matumla ambaye alikuwa bondia mahiri na aliyeshinda
mataji mawili ya dunia kwa nyakati tofauti.
Mbali na mabondia hao pia
Bondia Mada Maugo atapanda ulingoni kuzichapa na mpinzani wake Japhet
Kaseba, ambapo Wawili hao watapambana katika pambano la utangulizi kabla
ya Mohammed Matumla hajapanda ulingoni kumvaa Mchina.
![]() |
Add caption |