Azam FC imeitungua Stand United kwa mabao 4-0 katika mechi iliyopigwa leo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Azam FC imeshinda mchezo huo ikiwa inazihitaji mno pointi mno.
Azam FC inahitaji kushinda kila mechi kati ya zilizobaki kwa kuwa inataka ubingwa au nafasi ya pili.
Ilianza kupata mabao yake kupitia kwa Gaudence Mwaikimba na Bryan Mwajegwa katika kipindi cha kwanza.
Mwaikimba akaongeza bao la tatu katika dakika ya 62 kabla ya Farid Malik kufunga la nne katika dakika ya 89.