BAADA ya mechi za wikiendi iliyomalizika jana, msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara umebadilika isipokuwa kwa timu nne za juu.
Yanga wanaendelea kujikita zaidi kileleni baada ya jana kuongeza pointi tatu wakishinda mabao 3-1 dhidi ya Mbeya City fc uwanja wa Taifa na kufikisha pointi 46 katika mechi 21 walizoshuka dimbani.
Nafasi ya pili inashikiliwa na Azam fc wenye pointi 38 kwa mechi 29 walizocheza.
Nafasi ya tatu wapo wekundu wa Msimbazi, Simba wenye pointi 35 baada ya kucheza mechi 21.
kagera Sugar wanaocheza leo dhidi ya Ruvu Shooting wanashika nafasi ya nne kwa pointi 28 walizovuna katika mechi 21 walizocheza.
Mkiani kuna mabadiliko, Prisons waliotoka suluhu na Ndanda fc sasa wanashika nafasi ya pili kutoka mkiani wakiwa na pointi 21 sawa na wanaoburuza mkia Polisi Morogoro lakini Wajelajela wana wastani mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa.
Katikati kuna mabadiliko, baada ya Stand United kushinda jana sasa wanashika nafasi ya sita (6) wakijikusanyia pointi 27 katika michezo 21 waliyocheza mpaka sasa.
Baada ya Mbeya City kufungwa jana sasa wameporomoka mpaka nafasi ya 9 wakiwa na pointi 25 baada ya michezo 22.
MSIMAMO MZIMA BAADA YA VIPUTE VYA WIKIENDI HUU HAPA;

Standings

  Rnk   Team MP W D L GF GA +/- Pts  
  1   Young Africans 21 14 4 3 39 12 27 46  
  2   Azam 20 10 8 2 27 14 13 38  
  3   Simba SC 21 9 8 4 27 15 12 35  
  4   Kagera Sugar 21 7 7 7 19 20 -1 28  
  5   Mgambo JKT 20 8 3 9 17 19 -2 27  
  6   Stand United 21 7 6 8 18 23 -5 27  
  7   Coastal Union 23 6 9 8 16 23 -7 27  
  8   Ruvu Shooting 21 6 8 7 14 18 -4 26  
  9   Mbeya City 22 5 10 7 17 21 -4 25  
  10   Ndanda 22 6 7 9 18 24 -6 25  
  11   Mtibwa Sugar 21 5 9 7 20 22 -2 24  
  12   JKT Ruvu 22 6 6 10 16 22 -6 24  
  13   Tanzania Prisons 21 3 12 6 14 20 -6 21  
  14   Polisi Morogoro 22 4 9 9 13 22 -9 21

Advertisement

 
Top