Mbeya City FC inayonolewa na kocha bora wa Ligi Kuu ya Bara msimu uliopita, Juma Mwambusi, ilishinda 1-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya.’
  
NDANDA FC imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara baada ya leo jioni kulazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Mbeya City FC.
Kwa sare hiyo, Mbeya City FC imefikisha pointi 24 na kupanda kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya tisa ikizishusha Mgambo Shooting Stars na Mtibwa Sugar FC zenye pointi 23 kila moja wakati Ndanda FC imepanda kutoka nafasi ya 12 hadi ya nane ikifikisha pointi 24 pia.
Bao la wenyeji Ndanda FC limefungwa na mchezaji wa zamani wa Simba SC, Kiggi Makasy dakika ya 24 kabla mshambuliaji wa zamani wa Kagera Sugar FC, Themi Felix akiisawazishia City dakika ya 60.

Advertisement

 
Top