HAJIBU-NA-NYOSSO
Nyoso (kulia) alifanya kazi nzuri kumzuia Ibrahim Hajibu siku waliposhinda 2-1 dhidi ya Simba mwaka hu
BEKI mahiri na mkongwe wa Mbeya City fc, Juma Nyosso amesema hakuna kulaza damu, huu ni muda wa kazi, mambo mengine ni kuweka pembeni.
Januari 28 mwaka huu Mbeya City iliifunga Simba mabao 2-1 uwanja wa Taifa Dar es salaam, lakini Nyoso alifanya tukio la aina yake ikimpapasa makalio mshambuliaji wa Simba, Elius Maguli.
Baada ya tukio hilo kubainika siku chache zilizofuata, Nyoso alifungiwa mechi 8 na mechi ya kwanza kucheza baada ya kifungo hicho ilikuwa dhidi ya Azam waliyotoka 1-1 na Azam fc uwanja wa Azam Complex katikati ya wiki iliyopita.
Kuelekea  katika mechi hiyo, Nyoso amesema ni wakati mwingine mzuri wa kuwaonesha Simba kuwa yeye ni beki mgumu.
“Simba hakika nitawazuia kwa kushirikiana na wenzangu, wana wachezaji wasumbufu kama Okwi (Emmanuel), Hajibu (Ibrahim) na wengine, lakini nimejipanga kumficha hasa Okwi ambaye ni mtu hatari”. Amesema Nyoso.
Baada ya Okwi kuambiwa tambo hizo amejibu kuwa: “Ligi ni ngumu, wapinzani wananikamia, lakini siku zote natafuta mbinu mpya za kuwatoka. Niko tayari kupambana kwa ajili ya timy yangu ya Simba”.
Nyoso amewahi kuichezea Simba siku za nyuma na Coastal Union uliopita alikuwa Coastal Union

Advertisement

 
Top