TAARIFA mbaya kwa mashabiki wa Yanga na wapenda soka wanaoitakia mema timu hiyo katika mechi ya jumamosi dhidi ya Etoile du sahel ya Tunisia ni kwamba mshambuliaji hatari, Mrundi, Amissi Tambwe amezua hofu katika kambi ya klabu hiyo iliyopo Hoteli ya Tansoma Dar es salaam baada ya kuugua ghafla maleria.
Daktari wa Yanga, Juma Sufiani ameuambia mtandao huu muda mfupi uliopita kuwa bado haijulikani kama Tambwe anaweza kuikosa mechi ya hatua ya 16 bora ya kombe la Shirikisho dhidi ya Etoile.
Tambwe hajahudhuria mazoezi ya leo jioni yaliyofanyika uwanja wa Taifa Dar es salaam.
