Yanga imefuzu katika hatua ya pili ya michuano ya Kombe la Shirikisho ikiwa na timu nyingine 15.
Timu hizo 15 zinatokea katika mataifa 11 ambayo yana upinzani mkubwa wa kisoka.
Mataifa hayo ni Mali, Algeria, Misri, Nigeria, Gabon, Swaziland, Ivory Coast, Ghana, Tunisia, DR Congo na Morocco.
Yanga inakutana na Etoile du Sahel ya Tunisia katika raundi hiyo.
Kikosi hicho cha Mholanzi, Hans van der Pluijm kimefuzu baada ya kuing’oa FC Platnum ya Zimbabwe.