Kiungo nyota aliyetamba na Mbeya City, Deus Kaseke sasa ni mali ya Yanga.

KAseke amejiunga baada ya kuingia mkataba wa kuichezea timu hiyo jana.

Mabingwa hao walikuwa wakipambana kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya michuano ya kimataifa.

KAseke amejiunga na Yanga baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili, jana.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zimeeleza, Kaseke amemaliza na uongozi wa Yanga jana, hivyo sasa ni mali ya Jangwani.

Kabla ya hapo, kulikuwa na taarifa za kiungo huyo kuwaniwa na Yanga na Azam FC.

Simba walikuwa wa kwanza kutaka kumsajili msimu uliopita, lakini zoezi hilo likakwama.


Meneja wake, naye alilizungumzia msimu huu baada ya kusema walikuwa wakizungumza na Yanga na walifikia hatua nzuri zaidi.

Advertisement

 
Top