simba-vs-azam_bongoonetz
Macho na masikio ya wapenda soka hususani ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kesho itakuwa ni katika mchezo kati ya Simba SC pamoja na Azam FC mtanange utakaopigwa jioni ya saa kumi katika Uwanja wa Taifa huku ukitazamiwa kuwa na mashabiki wengi ambao watakuwa na hamu ya kuutazama moja kwa moja na wengine wakifatilia kupitia runinga na Radio mbalimbali.
bongoonetz_okwi
Kikubwa katika mchezo huu ambacho kinafanya kuwa wa kuvutia sana ni kutokana na nafasi inayowaniwa na timu zote mbili licha ya kutokuwa katika kiwango kizuri kimchezo uwanjani huku zikizidiana pointi nne kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Azam FC ambao sasa wamepokonywa ubingwa na Yanga SC baada ya kufikisha alama 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwenye ligi hiyo, kwa sasa wanawania nafasi ya pili ili waweze kupata uwakirishi wa Taifa katika michuano ya Kimataifa (Kombe la Shirikisho Afrika) wakiwa na pointi 45, sambamba na Simba wenye alama 41.
Januari 24 timu hizo mbili zilikutana katika Uwanja wa Taifa ambapo Azam walikuwa wenyeji, mwisho wa siku ziligawana pointi baada ya sare ya kufungana 1-1 kazi ya Emanuel Okwi pamoja na Didier Kavumbagu.
MICHEZO MINNE ILIYOPITA
Katika michezo sita ya mwisho ambayo Simba imecheza imefanikiwa kushinda minne na kupoteza miwili ambapo March 18 ilifungwa na JKT Mgambo kwa jumla ya mabao 2-0, March 21 Simba wakashinda 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting, April 6 wakaifunga Kagera Sugar 2-1, April 18 wakafungwa na Mbeya City 2-0, April 22 wakaifunga JKT Mgambo 4-0 na mwisho April 25 wakaifunga Ndanda 3-0.
Azam FC wao katika michezo sita iliyopita wameshinda michezo mitatu na kutoa sare tatu kitu ambacho kinaonyesha kuwa safu ya Ufungaji ya Azam inamatatizo katika kufumania Nyavu tofauti na wapinzani wao Simba.
March 22 Azam waliifunga bao 1-0 Coastal Union, April 8 wakatoa sare na Mbeya City 1-1, April 11 Azam wakatoa sare na Mtibwa Sugar 1-1, April 15 JKT Mgambo wakakomaa sare ya 0-0 kabla ya April 18 kuifunga Kagera Sugar 2-1, na Stand United kupigwa kwa bao 4-0. Kufatia takwimu hizo moja kwa moja unaweza kusema Simba wanashinda mchezo wa kesho lakini dakika 90 ndio zitaongeo na kutoa mshindi.
Katika michezo yote sita ambayo Azam FC imefanya vibaya Washambuliaji wake mahiri Kipre Tchetche pamoja na Nahodha wake John Bocco walikuwa nje wakiugulia majeruhi kitu ambacho kilipelekea safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo kuteteleka, Lakini kitu kizuri kwao katika mchezo huu wa kesho ni ujio wa nyota hao ambao wamereje vyema, Kipre aliingia dakika za mwisho dhidi ya Stand na Kutoa pasi ya goli huku akipewa nafasi ya kuanza kesho, John Bocco ambaye pia amekuwa na bahati ya kuwafunga Simba naye ananafasi kubwa ya kucheza baada ya afya yake kuimarika.
UWEZO BINAFSI WA WACHEZAJIbocco_bongoonetz
Ukiangalia timu zote mbili zinawachezaji ambao sio wa kuchezea katika eneo la hatari kwani muda wowote na mpira wa aina yoyote wanaweza kufunga mabao katika eneo lolote, Okwi ni mchezaji ambaye akiwa na mpira anauwezo wa kufanya chochote anachojisikia, anaweza kupiga chega kukimbiza ikiwa ni pamoja na kutoa pasi ya goli au yeye mwenyewe kufunga bao, mbali na Mganda huyo kuna wazawa kama Ibrahim Ajibu ambaye ana hat-trik mbili hadi sasa katika ligi ni mchezaji mwenye uwezo wa juu.
Mabao mengi ya Azam katika msimu huu yamekuwa yakitengenezwa na Kipre Tchetche pamoja na Briany Majwega ambao wanakimbiza pembeni na kuingia ndani mwisho wa siku wanatoa pasi kwa kavumbagu ambaye amekuwa hawaangushi, Uwepo wa Nyota hawa watatu na pengine kama ataingia John Bocco mwenye uzoefu mkubwa basi chochote kinaweza kutokea kutokana na uwezo wao wa kumiriki mpira, Nguvu na akili ya ziada wakiwa Uwanjani, bila shaka naamini hakuna anayepinga juu ya uwezo wa Kipre, Majwega, Kavumbagu na Bocco.
LAZIMA MMOJA AFUNGWEaazam
Mchezo huu kwa namna moja au nyingine ni mgumu kwa timu zote kwani Simba anapointi 41 akishinda mhezo wa leo atafikisha alama 44 na mchezo wa mwisho anacheza na Ruvu Stars ambapo akishinda atafikisha pointi 47 huku akiiombea mabaya Azam katika michezo yake yote iliyobaki iweze kupoteza na kubakia na alama zake 45.
Kwa Upande wa Azam FC wao kesho wakishinda basi wanakuwa wamejihakikishia nafasi ya pili kwa kufikisha alama 48 ambazo hata Simba ishinde mechi zote haitaweza kuzifikia, baada ya mchezo huo mabingwa hao wa mwaka jana watakutana na Yanga kabla ya kumaliza ligi na JKT Mgambo.
Yote kwa yote kesho tunategemea kutazam mchezo ambao utakuwa wa nguvu na wakuvutia, timu zote zikishambuliana ili kupata ushindi muda huo huo wakikaba kuzuia bao.
MWISHO

Advertisement

 
Top