Kocha mpya wa Simba, Dylan Kerr amewasili jijini Dar es Salaam amesema atapambana kuhakikisha Simba inafanya vema.


Kerr raia wa Uingereza amewasili jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Simba, Collins Frisch.

“Sijui vitu vingi kuhusiana na soka la Tanzania lakini lengo ni kutengeneza kikosi bora chenye kuleta ushindi.

“Kwa sasa inaweza kuwa mapema sana kuzungumzia mambo mengi, lakini najua tutafanikiwa tukishirikiana.

“Simba ni timu kubwa na maarufu, hivyo ushirikiano utakuwa nguzo ya kufikia mafanikio,” alisema.

Kocha huyo anachukua nafasi ya Goran Kopunovic raia wa Serbia ambaye Simba iliamua kuachana naye baada ya kutaka Sh milioni 100 ili asaini mkataba wa miaka miwili.
AKIWA NA KAIBU KATIBU MKUU WA SIMBA ALIYEMPOKEA.

Advertisement

 
Top