![]() |
| NGOMA AKISAINI... |
Hatimaye mshambuliaji nyota kutoka Zimbabwe, Donald Ngoma amesaini miaka miwili kuichezea Yanga.
Ngoma pamoja na kiungo Joseph Zuttah 'Tetteh' naye amesaini miaka miwili kuichezea Yanga.
![]() |
| TETTEHWote wawili jana walifanyiwa vipimo vya afya na kufuzu. Leo wakafanya mazoezi na kikosi cha Yanga kabla ya kusaini mkataba leo. |
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga, Isaac Chanji kwa kushirikiana na Katibu Mkuu, Dk Jonas Tiboroha ndiyo walishirikiana kukamilisha zoezi hilo.

