John Bocco ‘Adebayo’ na Kipre Tchetche wameipeleka Azam kwenye hatua ya robo fainali baada ya kila mmoja kufunga goli kwenye mchezo wa leo kati ya Azam FC dhidi ya Malakia ya Sudan Kusini ikiwa ni mwendelezo wa michuano ya Kagame Cup ambapo Azam ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0.
Bocco alianza kuifungia Azam goli la kuongoza dakika ya 27 kipindi cha kwanza kwa mpira wa adhabu ndogo nje kidogo ya eneo la hatari la Malakia goli lililoipeleka Azam mapumziko ikiwa mbele kwa goli 1-0.

Azam walitawala sehemu kubwa ya mchezo huo huku mchezaji wao mpya Jean Mugiraneza waliemsajili kutoka APR FC ya Ruanda akionekana kuimudu vyema nafasi ya kiungo wa ulinzi hali iliyosababisha punguza mashambulizi ya mara kwa mara kwenye lango la Azam.

Mchezo wa awali uliopigwa saa nane mchana kwenye uwanja wa taifa kati ya Al Shandy (Sudan) dhidi ya LLBA FC (Burundi) ulimalizika kwa sare ya kufungana goli 2-2.
Kikosi cha Azam kilichoanza: Aishi Mnula, John Bocco ‘Adebayor’, Pascal Wawa, Agrey Morris, Shomari Kapombe, Salumu Abubakar, Frank Domayo, Ame Ali, Jean Mugiraneza, Kamagi Gadiel Michael, Kheri Abdallah Salum