
PICHA ALIYOITUPIA MACHUPPA MTANDAO IKIMUONYESHA LOWASSA NA VIONGOZI WENGI WA JUU WA CHADEMA.
Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Athumani Machuppa ‘Mani’ ameonyesha wazi hisia zake kutokana na taarifa za kuwa mwanasiasa mkongwe wa CCM, Edward Lowassa anahamia upinzani.
Machuppa anayeishi nchini Sweden ametupia picha aliyoiunganisha kutoka mtadao wa kijamii wa Twitter na kuiweka Facebook huku akisema: “madaraka haya”.
Katika maelezo yake, Machuppa anaonyesha kushangazwa na Lowassa kuhamia Ukawa ambao wapinzani ndiyo waliomuita fisadi.
MACHUPPA.
Asilimia 90 wanaonekana kumuunga mkono Machuppa huku wakishangazwa na Lowassa anayeungana na waliomuita fisadi na mwizi.
Lakini wengine wanamuunga mkono Lowassa kwamba CCM zaidi ya miaka 50 sasa hawajaleta maendeleo.
Mwisho Machuppa anonyesha kuhoji, kwamba kama hakuna maendeleo, Lowassa atayaleta? Swali lake linaonekana kuwa gumu.
Taarifa hiyo huku picha inaonekana Lowassa akiwa na viongozi wa Chadema imezua stori nyingi mtandaoni na watu wanajadili hasa suala la wapinzani kumtangaza Lowassa ni fisadi na sasa wanakubali awe mgombea wao wa urais?