
Vincent
Bossou (kulia) akipambana na Didier Drogba wakati wa michuano ya kombe
la Mataifa ya Afrika (CHAN) mechi iliyokuwa kati ya Togo na Ivory Coast
kwenye dimba la Royal Bofokeng Stadium Januari 22, 2013 Rustenburg,
Afrika Kusini
Leo asubuhi Yanga imemsajili beki
wa kati Vicncent Bossou ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Togo
ikiwa bado masaa machache kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili
ambapo dirisha hilo litafungwa leo saa 6:00 usiku.
Beki huyo alianza soka lake
kwenye klabu ya Maranatha FC mwaka 2006 na kudumu kwenye klabu hiyo
mpaka mwaka 2009 akicheza jumla ya mechi 77 na kuifungia klabu hiyo
magoli matano (5).

May 2011 Bossou alijiunga na
klabu ya Navibank Saigon F.C ya Vietnam ambapo alicheza mechi 35 akiwa
na timu hiyo na kufanikiwa kufunga magoli matatu (3) na kwa sasa alikuwa
na mkataba na klabu ya Govang Hi FC ya Korea Kusini.
Bossou alikuwepo kwenye kikosi
cha Togo ambacho kilijitoa kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka
2010 baada ya basi la timu hiyo kushambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa
ni magaidi wakati wanawasili nchini Angola ambako ndipo mahindando hayo
yalifanyika kwa mwaka huo wa 2010.
Ameshaichezea timu ya taifa ya Togo kwenye michezo ipatayo 25 hajafanikiwa kufunga goli hata moja kwa mechi zote alizocheza.
Wasifu wake
Taarifa binafsi:
Jina kamili: Vincent Bossou
Tarehe ya kuzaliwa: Februari 7, 1986 (miaka 29)
Sehemu alikozaliwa: Kara, Togo
Urefu: mita 1.86 (futi 6 na inchi 1)
Nafasi anayocheza: Beki wa kati
Taarifa zinazo husu klabu
Klabu anayocheza sasa: Yanga
Orodha ya timu ambazo amewahi kucheza, idadi ya mechi alizocheza na magoli aliofunga.
Mwaka | Timu | Mechi alizocheza | Magoli aliyofunga |
2006-2009 | Maranatha FC | 77 | (5) |
2010 | ES Sahel | 3 | (0) |
2010-2011 | Maranatha FC | 23 | (3) |
2011-2012 | Navibank Saigon | 35 | (1) |
2013 | Becamex Binh Durong | 1 | (0) |
2013 | TDC Binh Durong | 17 | (0) |
2014 | An Giang | 21 | (0) |
2015 | Goyan Hi FC | 0 | (0) |
2010- | Togo | 25 | (0) |
Yanga wamemsajili beki huyo kwa
ajili ya kuiongezea nguvu safu yao ya ulinzi ambayo kwa muda mrefu
imekuwa ikitumikiwa na mabeki wawili Nadir Haroub ‘Canavaro’ na Kelvin
Yondani ambao ubora wao unapungua kutokana na kucheza mechi nyingi
kwenye timu hiyo bila kupumzika.