
Sehemu ya mkataba huo inaeleza kiasi cha shilingi za kitanzania Bilioni 1.2 kinakwenda moja kwa moja kwenye klabu 16 ambazo zitapapatuana kwa ajili ya kuuwani ubingwa wa Tanzania bara msimu wa 2015-2016.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa kampuni ya Vodacom Tanzania Kelvin Twisa, amesema hatua ya kutiliana saini na TFF kupitia bodi ya ligi, inaendelea kudhihirisha uhusiano mzuri uliopo kati yao ikiwa ni pamoja na dhamira ya kutaka kulivusha soka la Tanzania na kulipeleka mbali zaidi.