Bahanuzi-in-Stars
Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaa
Mabingwa wa zamani wa ligi kuu Tanzania baratimu ya Mtibwa Sugar,  imewarejesha kundini ‘mastraika’ Said Bahanunzi na Hussein Javu ambao walifanya vizuri katika klabu hiyo kabla ya kutimkia Yanga SC.
Bahanunzi alifunga mabao nane msimu wa 2011/12 kisha akasajiliwa Yanga, Javu akachukua nafasi yake na kuwa mfungaji namba moja katika timu hiyo msimu wa 2012/13 naye akatimkia Yanga mara baada ya kumalizika kwa ligi.
Baada ya kuwapoteza washambuaji Jamal Mnyate aliyemaliza mkataba wake na kujiunga na Mwadui FC ya Kahama, Musa Hassan Mgosi aliyejiunga na Simba SC, kocha mkuu wa timu hiyo, Mecky Mexime amesema kuwa washambuaji hao watafanya vizuri kushirikiana na vijana kama Ally Shomari kuifanya Mtibwa kuwa ‘moto’ msimu huu.
“Ni kweli tumewasaini Javu na Bahanunzi kwa kuwa ni wachezaji wenye uwezo wa kuisaidia timu yetu” amesema Mecky Mexime ambaye kikosi chake kitawavaa Stand United katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu bara siku ya Jumamosi katika uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
“Tulipoteza michezo miwili katika uwanja wa Kambarage msimu uliopita (dhidi ya Kagera Sugar na Stand) tumejiandaa kuwakabili Stand. Timu ipo vizuri naimani tutaanza msimu vizuri”.
Anaongeza kusema Mecky ambaye pia amemrejesha mlinda lango aliyeshindwa kutulia Simba SC, Hussein Sharrif. Mtibwa iliifunga Stand 3-1 katika mchezo wa kwanza msimu uliopita lakini ikachapwa 1-0 katika uwanja wa Kambarage katika gemu ya marejeano.

Advertisement

 
Top