Aliyekuwa Kocha wa viungo wa Simba, Dusan
Momcilovic ‘Dule’ raia wa Serbia, amepata dili ambapo sasa anainoa timu ya OFK
Beograde inayoshiriki Ligi Kuu ya Serbia.
Hata hivyo wakati akiondoka, Dule alisema lazima Simba itafungwa na Yanga katika mchezo wake uliokuwa unafuata.
Dule aliyeondoka nchini mwishoni mwa Oktoba,
mwaka huu, alikuwa ana kazi maalum ndani ya kikosi cha Simba ya kuwajengea
stamina wachezaji wa timu hiyo, kazi aliyoifanya kwa miezi mitatu kabla ya
mkataba wake kumalizika mwezi huo.
Akizungumza kutoka Serbia, Dule alisema mara baada ya kumalizana na Simba, alirejea
nyumbani kwao ambapo kwa siku chache tangu afike huko akapata dili hilo.