Nafasi walioipata Mbeya City msimu huu ni nafasi moja chini ya walioipata mwaka jana ambapo ndio ilikua msimu wao wa kwanza wa ligi kuu.
Kocha mkuu wa kikosi hicho Juma Mwambusi alipewa tuzo ya kocha mwenye mafanikio na mstahimilivu kwa misimu miwili na kuiweka timu katika nafasi nzuri mfululuzo.
Wachezaji Paul Nonga, Themi Felix na Deus Kaseke walipata tuzo za heshima kwa mchango wao kwenye timu kwa misimu miwili.
Golikipa aliyekuja kuziba nafasi ya David Buruani, Hamilton Kalyesibula amepewa tuzo ya kipa bora akiwazidi wenzake.
Mkongwe Juma Nyosso, Hassan Mwasapili na Peter Mwalihanzi wao wamepewa tuzo ya uchezaji bora hususani mzunguko wa pili.
Lakini wachezaji wengine 18 wamepewa zawadi mbalimbali sambamba na fedha taslim.
Hata hivyo timu hiyo kupitia kwa afisa habari wake Dismas Ten imeipongeza timu ya yanga kwa kuwa mabingwa wa ligi hiyo na kuwataka wajipange vilivyo kwa michuano ya kimataifa mwakani.v