Dk Hemant Kalyan wa nchini India amesema upasuaji wa Kiongera ulifanyika kwa mafanikio makubwa.

"Kweli daktari ambaye ni bingwa katika upasuaji amethibitisha. Katuambia Kiongera atarejea vizuri," kilieleza chanzo.

Kiongera anatarajia kurejea wiki ijayo baada ya matibabu hayo.

Simba inaendelea kumlipa mshahara mshambuliaji huyo wa zamani wa KCB ya Kenya lakini ilimuondoa kwenye usajili na nafasi yake kuchukuliwa na Mganda, Danny Sserunkuma.
Daktari nguli aliyemtibu mshambuliaji wa Simba, Paul Kiongera amewatoa hofu Msimbazi na kuwaambia Mkenya huyo atarejea na kucheza soka.

Advertisement

 
Top