BAADA ya kufanuikisha usajili wa kishindo wa mshambuliaji Mganda Dan Sserunkuma, Kamati ya Usajili ya Simba SC imesema haitamsajili kiungo Mgambia Omar Mboob kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Zacharia Hanspope amesema jijini Dar es Salaam leo kuwa ujio wa Sserukumba umeziba nafasi ya mchezaji mwingine wa kigeni kusajili Simba SC.
Sserunkuma aliyesaini mkataba wa miaka miwili jijini leo kuitumikia Simba, amepishwa na mshambuliaji Mkenya Paul Kiongera ambaye mkataba wake umesitisishwa hadi pale atakapopatiwa matibabu ya goti lake nchini India.
“Hatutasajili tena mchezaji wa kigeni kipindi hiki cha dirisha dogo baada ya kumpata Sserunkuma. Mboob ni kwa ajili ya msimu ujao lakini kama akionesha kwamba ni mkali zaidi, tutazungumza na wachezaji wengine wa kigeni tulionao tuone yupi yuko tayari kuvunja mkataba,.

“Watu hawafahamu vyema kuhusu ujio wa Mboob Simba. Mimi nilikutana na meneja wake katika shughuli zangu za kibiashara akaniambia kijana wake ni mzuri na muda wowote atakwenda kufanya majaribio barani Ulaya. Nikaona si mbaya akaja hapa tukamwangalia,” amesema Hanspope.
Mbali na Sserunkuma, Simba pia ina wachezaji wengine wanne wa kigeni ambao Waganda Emmanuel Okwi na Joseph Owino pamoja na Warundi Pierre Kwizera na Amissi Tambwe.
Mboob yupo jijini akifanya majaribio kulishawishi benchi la ufundi la Simba chini ya Mzambia Patrick Phiri ili asajiliwe lakini itakuwa ngumu kwa Phiri kumwachia mmoja kati ya nyota wake wanne waliokutwa na Sserunkuma Simba kwa vile Mboob ahajacheza mechi yoyote ya mashindano.
Dirisha dogo la usajili lilifunguliwa Novemba 15, mwaka huu na zimebaki siku 12 kabla ya kufungwa kwake.