KAMATI ya usajili ya Simba imeshindwa kupata beki wa kati kama walivyoagizwa na kocha mkuu, Mzambia, Patrick Phiri.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili
ya Simba sc, Zacharia Hans Poppe ameuambia mtandao huu kuwa kocha Phiri
aliagiza apatikane beki wa kati wa kiwango cha juu, lakini wameshindwa
kupata beki wa aina hiyo katika kipindi hiki cha dirisha dogo la
usajili.
Poppe aliongeza kuwa inabidi kocha aendelee na mabeki waliopo kwa sasa.
Kepteini huyo wa zamani wa JWTZ
aliongeza kuwa kocha aliagiza apatikane mshambuliaji mkali na
wamefanikiwa kumsainisha miaka miwili nyota wa Gor Mahia ya Kenya,
Mganda Danny Sserunkuma.
Aidha aliongeza kuwa wapo katika mazungumzo ya mwisho na nyota wa Polisi Morogoro Danny Mrwanda na Hassan Kessy wa Mtibwa Sugar.
Muda wowote kutoka sasa makubaliano na wachezaji hao yatafikiwa na kuwasainisha mikataba.