Uongozi wa Ndanda FC umewaambia Simba kuwa mechi yao ya Jumamosi si Mapinduzi Cup.



Simba iko mjini Mtwara kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Katibu Mkuu wa Ndanda, Edmund Njoweka amesema wanawasubiri Simba kwa hamu hiyo Jumamosi.

"Sawa tunawakaribisha Mtwara, ila wajue hii si Mapinduzi Cup, michuano ya kawaida tu. 

"Hii ni ligi na kweli tuko vizuri. Tumefanya vizuri dhidi ya Prisons, tumetoa sare na Polisi. Sasa tuko tayari kwa ajili yao.

"Kweli tuko nje ya mji kwa ajili ya maandalizi ya mechi hiyo na tumepania kushinda," alijigamba Njowoka.

Simba imetua Mtwara leo na ililazimika kuunganisha safari ikitokea Zanzibar ikiwa na lengo la kufika Mtwara mapema.

Tayari Simba imecheza mechi nane za ligi, imeshinda moja, sare sita na imepoteza moja ikiwa chini ya Kocha Patrick Phiri.

Mechi ya Jumamosi itakuwa ni ya kwanza kwa kocha Mserbia, Goran Kopunovic.


Advertisement

 
Top