KIKOSI cha Simba SC leo jioni kimefanya mazoezi Uwanja wa CCM Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara kujiandaa na mechi ya keshokutwa ya ligi kuu soka Tanzania katika uwanja huo dhidi ya wenyeji Ndanda fc ‘Mtwara Kuchele’.
Afisa habari wa Simba, Humphrey Nyasio amesema wachezaji wote wapo salama na kocha Goran Kopunovic ana matumaini makubwa ya kuchukua pointi tatu muhimu.
“Tumefanya mazoezi leo jioni, kocha amewaona wachezaji wake na akasema wapo fiti. Ndanda lazima wana hofu, wameona mambo makubwa tuliyofanya kombe la Mapinduzi”.