Yanga leo inatarajiwa kujitupa uwanjani kuvaana na Kagera Sugar katika kuuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara unaoshikiliwa na Azam FC.


Katika mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Yanga watashuka uwanjani wakiwa na pointi 31, nyuma ya Azam wanaoongoza wakiwa na 33.

Pluijm alisema kuwa wachezaji hao wataikosa mechi hiyo kutokana na matatizo mbalimbali ikiwemo kadi nyekundu, njano na ugonjwa.

Pluijm aliwataja wachezaji hao watakaoikosa mechi hiyo kuwa ni Haruna Niyonzima mwenye kadi ya nyekundu, Kelvin Yondani, Salum Makapu na Danny Mrwanda, wote wanatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Wengine ni Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aliyerejea jana uwanjani kwa kufanya mazoezi mepesi ya binafsi akisimamiwa na Charles Mkwasa baada ya kupasuka juu ya jicho na Andrey Coutinho anayesumbuliwa na goti.

“Mechi ya kesho (leo) timu yangu itaingia uwanjani bila ya wachezaji wangu sita ambao wote ni muhimu kwenye kikosi changu.


“Licha ya kuwakosa wachezaji hao, wapo wachezaji wengine wenye uwezo mkubwa wa kucheza soka na kupata matokeo mazuri, kikubwa ni kumuamini kila wachezaji,” alisema Pluijm.

Advertisement

 
Top