SIMBA wanazuru kituo cha soka cha aliyekuwa kocha msaidizi wa Taifa Stars, , Marehemu, Silverster Marsh kiitwacho ‘Marsh Soccor Academy” kilichopo jijini Mwanza.
Msemaji wa Simba, Hajji Sunday Manara ameeleza kuwa Simba ni timu ya watu na inathamini sana mchango wa Marsh Katika soka, hivyo watakwenda hapo ili kuwafariji vijana wanaolelewa katika kituo hicho.
Manara amesema Simba ni timu ya watu, kwa maana hiyo inathamini sana masuala ya kijamii.
Marsh ambaye amefariki mwishoni mwa mwezi February alikuwa moja ya makocha wa kiwango cha juu na alifariki baada ya kusumbuliw kwa muda mrefu na kansa ya koo.
Hata hivyo baada ya zoezi hilo, Simba kesho jumamosi itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya wenyeji wa uwanja wa CCM Kirumba, Toto African.
