KATIKATI ya wiki hii, Yanga na Azam walicheza mechi zao za ligi kuu Tanzania bara.
Yanga waliwafunga 8-0 Coastal Union uwanja wa Taifa Dar es salaam wakati Azam walitoka 1-1 dhidi ya Mbeya City fc uwanja wa Azam Complex.
Kabla ya mechi hizo, washambuliaji wawili, Simon Msuva (Yanga) na Didier Kavumbagu (Azam fc) walitambiana katika harakati zao za kuwania kiatu cha dhahabu.
Msimu uliopita, Amissi Tambwe alifunga magoli 19 na kuchukua kiatu hicho, lakini msimu huu mambo yamekuwa magumu kwake ingawa alifunga magoliu 4 katika ushindi wa Yanga wa 8-0 na kufikisha magoli 9.
Kavumbagu na Msuva wanachuana vikali kufunga magoli na kila mtu alisema nitafunga;
Yanga wakishinda, Msuva alifunga magoli mawili (2) wakati Kavumbagu alitoka mikono mitupu Azam ikitoa sare Chamazi.
Didier Kavumbagu
Kwa sasa Msuva bado yupo juu kwa magoli 13 akifuatiwa na Didier Kavumbagu na Rashid Mandawa wa Kagera Sugar FC akiwa na magoli 10, Amissi Tambwe akishika nafasi ya tatu kwa magoli 9.
Mwishoni mwa wiki hii Msuva na Kavumbagu wanacheza.
Azam wanacheza leo na Mtibwa Sugar Manungu Turiani. Kavumbagu anatarajia kuwaongoza Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu.
Kuelekea mechi hiyo Kavumbagu amesema: “Sikufunga mechi iliyopita, hakika sikutarajia. Maneno yangu ni yaleyale, mshambuliaji anajisikia furaha pale tu anapofunga. Msuva amenipa changamoto, alifunga mawili na kunizidi mawili, lakini magoli hayo kitu gani bwana? nitalipa leo kwa Mtibwa”.
Msuva yeye amesema: “Kesho tuna mchezo mgumu na Mbeya City, namshukuru Mungu tuko vizuri, ninajiandaa kuisaidia timu yangu kupata matokeo mazuri pia kufunga ili niendelee kuwa kiongozi wa wafungaji magoli.
“Hahahahaha! kaka unapenda kutuchonganisha na Kavumbagu eeeh? sema nafurahi kwasababu napata changamoto kwake, najua ananipumulia nyuma, malengo yangu ni kumuacha mbali. Kesho moto ni uleule tukiamka wazima”.
