11150198_368610266670119_6707735268238217996_n
KUNDI maarufu la Yanga Facebook Family leo asubuhi katika uwanja wa Karume, Ilala, Dar es salaam limekabidhi tuzo ya mchezaji bora wa klabu hiyo kwa Mrisho Khalfan Ngassa.
Ngassa amechaguliwa mchezaji bora kutokana na mchango wake mkubwa alioonesha mwaka huu klabuni hapo.
Pia Haruna Niyonzima amepewa tuzo ya mchezaji bora wa kigeni klabuni hapo wakati Simon Msuva amepewa tuzo ya mfungaji bora wa klabu mwaka msimu huu.
Yanga facebook family wakipiga picha ya pamoja na wachezaji leo karume baada ya kutoa tuzo mbalimbali kwa wachezaji wa klabu ya Yanga
Tuzo hizo zinakuja siku chache baada ya Yanga kuvunja rekodi ya msimu uliopita ya kufunga magoli mengi wakiifunga Coastal Union magoli 8-0 tofauti na kipigo cha 7-0 walichotoa kwa Ruvu Shooting msimu uliopita.
Msuva alifunga magoli mawili (2), Tambwe manne (4), Kpah Sherman (1) na Salum Telela (1).
Niyonzima hakufunga, lakini aliichezesha timu kwa ufundi mkubwa mno.
Haruna Niyonzima amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa kigeni na kikundi cha Yanga facebook family

Advertisement

 
Top