YANGA SC wanaongoza msimamo wa ligi kuu wakijikusanyia pointi 43 kileleni baada ya kucheza mechi 20.
Azam fc wanashika nafasi ya pili kwa pointi 37 baada ya jana kutoka sare ya 1-1 na Mbeya City uwanja wa Azam Complex katika mechi yao ya 19 msimu huu.
Matokeo hayo yamewafanya Azam fc waweke reheni ubingwa wao kutokana na mzigo walionao mbele yao licha ya kuwa na mchezo mmoja zaidi ukilinganisha na Yanga.
Yanga wamebakiza mechi 6 za ligi kuu ambazo ni:
Yanga v Mbeya City
Yanga v Polisi Moro
Yanga v Stand United
Yanga v Azam fc
Ruvu Shootings v Yanga
Ndanda fc v Yanga
Uwanja wa Taifa unawakubali Yanga kwa kiasi kikubwa wamepoteza mechi moja tu msimu huu katika uwanja huo, wakifungwa 1-0 na Simba machi 8 mwaka huu.
Lakini ugenini wamepoteza mechi mbili, 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar na 1-0 dhidi ya Kagera Sugar.
Katika mechi sita zilizosalia, mechi 5 Yanga anacheza uwanja wa Taifa na moja Mtwara, kwa jinsi Yanga wanavyouweza uwanja huu, kuna urahisi wa kuwafunga?
Azam fc wamebakiza mechi 7 ambazo ni
Mtibwa Sugar v Azam fc
Mgambo JKT v Azam fc
Azam fc v Kagera Sugar
Azam fc v Stand United
Azam fc v Yanga
Azam fc v Simba
Azam  fc v Mgambo JKT
Hebu niambie mdau, kwa muziki wa mechi zilizosalia kwa Yanga na Azam fc, nani anaweza kubeba kombe msimu huu?

Advertisement

 
Top