
SIMBA SC inamtumia kiungo wake
mshambuliaji Emmanuel Okwi katika mechi ya leo ya ligi kuu soka Tanzania
bara inayopigwa uwanja wa Taifa Dar es salaam dhidi ya Mgambo JKT.
Mechi ya kwanza iliyopigwa Mkwakwani, Mgambo walishinda magoli 2-0.
Simba wanaingia uwanjani wakiwa
na machungu ya kuchapwa 2-0 na Mbeya City katika mechi ya ligi kuu
iliyopigwa mwishoni mwa juma lililopita uwanja wa Sokoine, Mjini Mbeya.
Kuelekea katika mpambano huo,
Okwi aliyeikosa mechi iliyopita kwa kuwa na kadi tatu za njano amesema
atajitahidi kuisaidia timu yake ipate matokeo.
“Namshukuru Mungu tuko salama,
mimi na wachezaji wenzangu tuko katika morali kubwa. Tulipoteza mechi
Mbeya, hatujakata tamaa, leo tunapambana kupata pointi tatu”. Amesema
Okwi.
Wakati Okwi akiwa na matarajio
ya kupata ushindi, naye mshambuliaji nyota wa Mgambo JKT, Malimi Busungu
ambeya anawaniwa na Simba, Yanga amesema leo ni siku nyingine ya
kuonesha uwezo wangu.
“Hii ni mechi yangu muhimu
kuwaonesha tena watanzania uwezo wangu, nitapambana na kuhakikisha
nakuwa chachu ya ushindi, cha msingi dhuluma isiwepo, mechi hizi za
mwisho zina mambo yake”.