Simba imemaliza Ligi Kuu Bara kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu JKT.
Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar, leo. Mabao ya Simba yalifungwa na Wadhi Juma na Said Ndemla.
Simba inaendelea kubaki katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 47, tofauti ya pointi mbili na Azam FC walio katika pointi mbili ambao wamemaliza ligi wakiwa na pointi 49.