Na, Richard Bakana, Dar es salaam
Ligi kuu ya Soka Tanzania bara leo imefikia ukingoni kwa kushuhudia michezo saba tofauti katika mikoa sita tofauti, huku Mabingwa wapya wa ligi hiyo Dar es salaam Young Africans wakijikuta wanapokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Ndanda FC, Mtanange uliopigwa Mtwara katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Kufatia ushindi huo Ndanda wanakuwa wamefikisha pointi 31 na kujiondoa kwenye mkasa wa kushuka daraja.
Uwanja wa Taifa Simba ilikuwa ikiminyana na JKT Ruvu ambapo matokeo yamepatikana kwa Simba kuibuka na Ushindi wa bao 2-1.

Chamazi jijini Dar es salaam kunako uwanja wa Azam Complex, Wenyeji Azam FC wameweza kutoshana nguvu kwa kugawana pointi na Mgambo JKT baada ya kutoa sare ya bila kufungana.
Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM Kambarage kulikuwa na mchezo kati ya Wenyeji Stand United ambao waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting ambao wameshuka.



