AZAM WEB KAVU
“Kama kuna timu ilikuwa na mawindo kwa Didier Kavumbagu ihamishie sehemu nyingine, tumeamua kumuongezea mchezaji wetu kandarasi ya mwaka mmoja na msimu ujao ataendelea kuvaa jezi ya Azam fc”. Haya ni maneno ya katibu mkuu wa Azam fc, Idrissa Nassor ‘Father’ aliyosema usiku huu akithibitisha kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja, mshambuliaji wao , raia wa Burundi, Didier Kavumbagu.
Kavumbagu alikuwa anawindwa na Yanga kutokana na mapendekezo ya kocha mkuu wa mabingwa hao wa Tanzania bara, Hans van der Pluijm, lakini sasa dili limebumburuka baada ya Wanalambala kutegua mtego.
Hata katika kikosi chake bora cha msimu wa 2014/2015 wa ligi kuu soka Tanzania bara alichotaja Pluijm kupitia mtandao huu, alimuweka Kavumbagu na Amissi Tambwe katika nafasi za washambuliaji wawili wa kati.
Kavumbagu anaungana na Said Mourad, Erasto Nyoni na Salum Abubakar walioongezewa mikataba ndani ya kikosi hicho kinachotarajiwa kuanza kunolewa na kocha wake wa zamani aliyerejea tena,  Muingereza Stewart Hall.

Advertisement

 
Top