bongoonetz
Simba imeidungua Azam FC kwa mabao 2-1 na kufikisha pointi 44, ikiwa ni tofauti ya pointi moja dhidi ya Azam FC.
Azam FC iko katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 45.


Katika mechi ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba ilifanikiwa kupata bao lake la kwanza kupitia Ibrahim Ajibu, lakini Azam FC wakasawazisha mapema katika kipindi cha pili kupitia Mudathir Yahaya.

Wakati ikionekana kama mambo yamekuwa safi, Ramadhani Singano ‘Messi’ ambaye amekuwa akiinganyasa Azam FC kila mara alifunga bao safi kwa mkwaju aliouchonga kutoka nje ya 18.

Azam FC ilipata pigo kwa mchezaji wake Salum Abubakari ‘Sure Boy’ kulambwa kadi nyekundu kwa kummkanyaga Mohammed Hussein kwa makusudi kabisa.


Simba na Azam FC ndiyo timu zinazogombea nafasi ya pili huku tayari bingwa akiwa ameishatawazwa ambaye ni Yanga.




Advertisement

 
Top