Kocha wa Simba, Dylan Kerr, raia wa Uingereza, juzi aliushuhudia mchezo wa Yanga dhidi ya Gor Mahia dakika 90 lakini lilipokuja suala la kuzungumzia safu ya ulinzi ya Yanga, akalitaja jina la mshambuliaji wake mpya, Mganda, Hamis Kiiza.


Ingawa beki za Yanga zilicheza kwa ushupavu na bidii, lakini walipata shughuli kwa kujaribu kuwazuia mafowadi wenye majina makubwa Afrika Mashariki, Kagere Medie na Michael Olunga kabla ya kuruhusu mabao mawili na kuifanya mechi iishe kwa matokeo ya mabao 2-1.

Mchezo huo wa kwanza kwa Yanga katika michuano ya Kombe la Kagame 2015 ulipigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
KIIZA..
Kerr alisema: “Siwezi kuizungumzia Yanga kwa sasa, ni mapema, ndiyo kwanza michuano imeanza lakini nikwambie tu kwamba Simba tupo vizuri, nina timu nzuri na nina mafowadi wakali, ni vizuri tusubiri kukutana kwenye ligi.”

Alisema kwamba juhudi inayoonyeshwa na Kiiza ambaye ni mmoja wa mastraika wanaotajwa kwa sasa ni nzuri na inaonyesha kweli ana kitu atakachoinufaisha Simba msimu ujao.

“Nikwambie tu nina safu kali ya mafowadi na timu nzuri kiujumla, Kiiza ni mshambuliaji mzuri sana, ana vitu vingi na anaonyesha kweli jina lake kubwa linatokana na yeye alivyo uwanjani, tusubiri kuonana tu msimu ujao kwa sababu najua kila mmoja anajiandaa sasa.”

Advertisement

 
Top