Mwadui FC imesema inajitahidi sana kuomba mechi za kirafiki na klabu za Ligi Kuu Bara, lakini haizipati kwani kila timu inawagomea kujipima nayo.
Kilao amesema kuwa; “Tunahitaji michezo mingi ya kirafiki lakini kila tukiomba mechi kwa timu za ligi kuu tunakosa. Tumejaribu Toto African na Stand United kote imeshindikana, hivyo tunacheza na timu yoyote ili kujipima tu.”
Mwadui inayofundishwa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ imesajili nyota kibao waliowahi kucheza Simba na Yanga akiwemo Athuman Idd ‘Chuji’.