
Michezo mingine ya robofainali itaendelea siku ya Jumatano tarehe 29 Julai wakati wababe wa Kenya timu ya Gor Mahia itakapo pambana na Malakia FC ya Sudan Kusindi huku APR FC ya Rwanda ikichuana na Khartoum National Club ya Sudan.
Kutokana na ratiba hiyo, inamaanisha timu moja ya Tanzania kati ya Azam FC au Yanga lazima iyape mkono wa kwaheri mashindano hayo na kuipisha timu moja isonge mbele kwenye hatua ya nusu fainali.
Hii hapa ratiba kamili ya michezo ya robo fainali;
Al Shandy (Sudan) vs KCCA (Uganda)
Azam FC (Tanzania) vs Yanga (Tanzania)
Gor Mahia (Kenya) vs Malakia FC (Sudan Kusini)
APR FC (Rwanda) vs Khartoum National Club (Sudan)