Mabingwa wa soka Afrika
Mashariki na Kati, Azam FC wanaendelea kujifua Visiwani Zanzibar
kuelekea mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya timu ya Yanga ambayo itapigwa
Agosti 22 mwaka huu uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Afisa habari wa klabu hiyo,
Jafar Idd Maganga amewaambia waandishi wa habari kwamba kesho kutwa
(Agosti 12) kikosi chao kitacheza mechi ya kwanza ya kirafiki dhidi ya
KMKM.
Mchezo huo utakaopigwa uwanja wa Amaan Zanzibar utaanza majira ya saa 1:00 usiku
