Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Elius Maguri amesema hadi sasa hajajua sababu rasmi ya kuachwa na wekundu hao wa Msimbazi.
Kwa mujibu wa Maguri, amekuwa
akituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa viongozi wa Klabu hiyo ikiwa ni
pamoja na kuwapigia simu kutaka kujua hatma yake, lakini hapati majibu.
Maguri amefafanua kwamba
walipotoka Zanzibar ambako waliweka kambi ya wiki mbili, wachezaji
walitakiwa kuingia kambini kujiandaa na mechi ya Simba Day dhidi ya
Sports Club Villa ya Uganda, lakini jina lake halikuwepo kwenye orodha
ya wachezaji waliotakiwa kuingia kambini.
Taarifa za chini zinaeleza
kwamba, Simba inataka kumtoa kwa mkopo au kuvunja mkataba wake wa mwaka
mmoja kwasababu hayupo kwenye mipango ya kocha Dylan Kerr.
