
Kurudishwa kwa michuano hii
imekua ni faraja kwa wapenzi na wadau wa mpira miguu nchini baada ya
kukosekana kwa takribani miaka 13 michuano hiyo, ambapo sasa Bingwa wa
kombe la Shirikisho ataiwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la
Shirikisho Barani Afrika (CAFCC).
Akiongea na waandishi wa habari
wakati wa uzindizi wa michuano hiyo na kuchezeshwa droo ya awali, Rais
wa TFF Jamal Malinzi amemshukuru Mkurugenzi wa Azam Media Rhys
Thorrington kwa kuweza kudhamini michuano ambayo itongeza ushindani
zaidi nchini.
Malinzi amesema anaviomba vilabu
vitakavyoshiriki michuano ya kombe la hilo, vioneshe ushindani mkubwa
kwani ndio nafasi pekee ya kuweza kujitangaza na kuonekana kwa kuwa
michuano hiyo itakua ikionyeshwa moja moja na luninga ya Azam tv.
Aidha Malinzi amesema kila timu
inayoshiriki michuano hiyo itapata fedha ya usafiri shilingi milioni 3,
na vifaa vitakavyotolewa na mdhamini kampuni ya Azam Media.
Naye
Mkurugenzi wa Azam media Rhys Thorrington amesema udhamaini huo wa
miaka mine una thamani ya fedha za kitanzania bilioni 3.3 ambapo timu
zitakazoshiriki michuano hiyo zitapata nafasi ya kuonekana moja moja
katika nchi zaidi ya saba barani Afrika kupitia kituo chao cha Azam tv.

Timu zote 24 za ligi daraja la
pili na 8 za ligi daraja la kwanza 3, zilizopanda daraja na 5
zilizoshika nafasi za chini kwenye makundi yote zitashiriki katika
raundi ya kwanzamwezi Novemba kwa kucheza mechi 16 na kupata washindi 16
ambao wataingia raundi ya pili.
Timu 16 zilizoshinda raundi ya
kwanza na 16 zilizofanya vizuri ligi daraja la kwanza zitachanganywa na
kupangwa kucheza mechi 16 nyingine za raundi ya pili mwezi Desemba.
Washindi wa raundi ya pili
wataingia raundi ya tatu ambapo watachanganywa na timu 16 zilizopo ligi
kuu na kuchezwa mechi 16 nyingine ambazo washindi wake wataingia raundi
ya nne. Raundi hii ya tatu itafanyika mwezi Januari 2016.
Timu 16 zilizoshinda raundi ya
tatu zitaingia raundi ya nne zitapangwa ili kucheza hatua hii ambayo
itakuwa na mechi 8 na washindi 8 wataingia katika hatua inayofuata
ambayo ni raundi ya tano au robo fainali. Raundi hii ya nne itachezwa
Februari 2016.
Washindi wa raundi ya nne
watapata nafasi ya kuingia raundi ya 5 ambayo pia ni robo fainali, droo
itapangwa. Raundi hii ya tano itachezwa mwezi Machi 2016.
Washindi wa raundi ya tano au robo fainali watapangwa kucheza nusu fainali au raundi ya 6 mwezi Aprili.
Washindi wa nusu fainali
watapambana katika fainali na kumpata bingwa wa Azam Sports Federation
Cup 2015/16. Mechi ya fainali itachezwa wiki moja baada ya ligi kuu
kumalizika na Bingwa atakabidhiwa kombe na zawadi ya fedha tasilimu
shilingi milioni 50.
Mechi za raundi ya kwanza na
raundi ya pili kama mshindi hatapatikana ndani ya dakika 90 basi mshindi
atapatikana kwa kupigiana penati moja kwa moja. Mechi za raundi ya tatu
na nne kama mshindi hatapatikana ndani ya dakika 90 mechi itarudiwa
katika uwanja wa timu iliyokuwa mgeni mechi ya awali.
Mechi za robo fainali au raundi ya tano kama mshindi hatapatikana ndani ya dakika 90 hatua ya penati tano tano itaamua mshindi.
Kwa mechi za nusu fainali na
fainali kama mechi itaisha kwa sare ndani ya dakika 90, dakika 30 za
nyongeza zitachezwa, na kama hakutakuwa na mshindi penati zitaamua
mshindi.
Raatiba ya raundi ya kwanza:
AFC -Arusha Vs Polisi Mara,
Polisi -Tabora Vs Green Worries -Dar es salaam, Karikoo Lindi Vs
Changanyikeni -Dar es salaam, Mkamba Rangers –Morogoro Vs Mvuvuma –
Kigoma, Rhino Tabora Vs Allicane – Mwanza, Panone Kilimanjaro Vs Coca
Cola Mbeya, Polisi Morogoro Vs Mshikamo Dar es salaam, Sabasaba Morogoro
Vs Abajalo Tabora.
Magereza Iringa Vs Polisi Dar es
salaam, Milambo Tabora Vs Town Small Ruvuma, Abajalo Dar es salaam Vs
Transit Camp Dar es salaam, Ruvu Shooting Vs Cosmopolitan Dar es salaam,
JKT Rwamkoma Mara Vs Villa Sqaud (Dar es salaam), Wenda FC Mbeya Vs
Madini Arusha, Pamba FC Mwanza Vs Polisi Dom, Singida United Vs
Bulyanhulu FC Shinyanga.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)