
Baada ya sare hiyo ya bao 1-1, tayari Mgambo imerejea fasta mjini Tanga kuiwahi Simba.
Imeanza mazoezi leo jioni kwa ajili ya mechi yao ya pili ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba kwenye
Baada ya kuanza Ligi Kuu Bara kwa kuitwanga African Sports, Simba imeendelea na mazoezi kwa ajili ya kazi nyingine kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini hapa, keshokutwa.
Itakuwa na kazi dhidi ya Mgambo ambao wamekuwa wabishi kila wanapokutana nao.
Simba chini ya Muingereza Dylan Kerr, inataka kufuta ugumu wa Mgambo ambao pia wako mjini hapa baada ya kuwasili mapemaa wakitokea Mtwara walipokwenda kupambana na Ndanda FC.