Kikosi cha Azam FC kilichocheza mechi ya Jumamosi dhidi ya Tanzania Prisons
Kikosi cha Azam FC kilichocheza mechi ya Jumamosi dhidi ya Tanzania Prisons
Timu ya ‘wanalamlamba’ Azam FC baada ya kupata ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex, tayari wameshatua mjini Shinyanga jana usiku kuikabili timu ya Stand United kesho kwenye uwanja wa CCM Kambaregae mjini Shinyanga.
Msemaji wa timu hiyo Jafar Idd amesema, timu iliondoka jana jijini Dar es Salaam kwa usafiri wa ndege hadi Mwanza na baadae kuchukua usafiri wa basi kuelekea Shinyanga kwa ajili ya mchezo wao wa Jumatano.
“Mwalimu amesema anafahamu kama Stand walipoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wao wa nyumbani lakini akasema maandalizi ndiyo yataamua nani atapata pointi tatu kwenye mchezo huo”.
“Tumeondoka na kikosi kizima, tumemwacha Balou pekeake ambaye ni majeruhi lakini wengine wote waliobakia tumesafiri nao”.
Stand United ‘chama la wana’ ilikufa kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Kambarage itataka kulazimisha kupata ushindi mbele ya Azam FC iliyoshinda mchezo wa kwanza dhidi ya Tanzania Prisons siku ya Jumamosi.

Advertisement

 
Top